News

Posted On: Jul, 19 2022

MWENGE WA UHURU WAPONGEZA MRADI WA MAJITAKA WA MWAUWASA

News Images

MWENGE WA UHURU WAPONGEZA MRADI WA MAJITAKA WA MWAUWASA

Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru 2022, Sahili Geraruma ameipongeza MWAUWASA kwa utekelezaji wa mradi wa Mfumo Rahisi wa Uondoshaji wa Majitaka maeneo ya milimani na ameitaka kutanua wigo wa mradi ili kunufaisha wananchi wengi zaidi.

Ametoa pongezi hizo Julai 17, 2022 wakati akizindua mradi wa Mfumo Rahisi wa Majitaka kwenye makazi ya miinuko katika eneo la Igogo-Sahara, Wilayani Nyamagana.

Mradi wa ujenzi wa Mfumo Rahisi wa Uondoaji Majitaka kwenye makazi ya miiunuko umetekelezwa katika maeneo ya Kabuhoro, Ibungilo, Isamilo na Igogo-Sahara kwa gharama ya shilingi 3,844,768,482.50.

"Mradi ni mzuri, pongezi kwenu MWAUWASA, mmefanya kazi kubwa na nzuri, Nyamagana ni safi, mhakikishe pia mnatanua mradi ili wananchi wengi zaidi wafikiwe," alisema Geraruma.

Aidha, aliwasisitiza wananchi kuacha tabia ya kutiririsha majitaka ovyo na badala yake wachangamkie kuunganishwa kwenye mfumo.

"Tabia ya kusubiri mvua inyeshe kisha mnazibua vyoo hii haifai. Muwaone MWAUWASA wawaelekeze nini cha kufanya ili muunganishwe kwenye huu mfumo,"alisisitiza

Mradi unatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Washirika wa Maendeleo ambao ni Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kupitia mkopo wa masharti nafuu lengo likiwa ni kupunguza utiririshaji wa majitaka kutoka majumbani kuelekea Ziwa Victoria ambayo kwa kiasi kikubwa husababisha uchafuzi wa maji ya Ziwa ambalo ndio chanzo kikubwa cha maji kwa wakazi wa mwambao wa Ziwa