News

Posted On: Jul, 19 2022

TENKI LA MAJI MLIMA WA RADA LAZINDULIWA

News Images

TENKI LA MAJI MLIMA WA RADA LAZINDULIWA

Mwenge wa Uhuru 2022 umezindua mradi wa maji katika eneo la Mlima wa Rada Kata ya Kiseke Wilaya ya Ilemela wenye thamani ya Shilingi 365,580,080.00.

Ujenzi wa mradi umefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19

Akizindua mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2022, Sahili Geraruma aliwataka wanufaika kuhakikisha wanatunza miundombinu yake kwa manufaa yao na vizazi vijavyo.

Mradi huo utasaidia kupatikana kwa huduma za maji ndani ya Kata ya Kiseke hususan kwa wakazi wa eneo la Mlima wa Rada ambapo utanufaisha jumla ya wakazi 3,600 na hivyo kuongeza kiwango cha upatikanaji wa majisafi na salama kwa wakazi wa maeneo husika.