​​TAARIFA YA DHARURA: HITILAFU YA BOMBA KUBWA KONA YA BWIRU

Posted On: Aug 28, 2023


TAARIFA YA DHARURA: HITILAFU YA BOMBA KUBWA KONA YA BWIRU

Kumetokea hitilafu ya Bomba kubwa la maji (inchi 20) na kusababisha maeneo ya Kilimahewa, Selemani Nasor, Nyamanoro, Pasiansi, Iloganzara, Ilemela, Lumala, Kiseke yote, Mondo, Bwiru, Kitangili, baadhi ya maeneo ya Buswelu na baadhi ya maeneo ya Kirumba kukosa huduma ya maji.

Jitihada za kuhakikisha hitilafu inadhibitiwa zinaendelea kwa kasi ili kurejesha huduma kwenye hali yake ya kawaida mapema.

Matengenezo yanatarajiwa kukamilika saa 12:00 Jioni

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliyojitokeza

Imetolewa Tarehe 28 Agosti, 2023 na:-

………………………………….

OFISI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO

MWAUWASA

Upatapo taarifa hii, tafadhali mfahamishe na mwingin