Zoezi la Uhakiki wa Wateja

Posted On: Aug 03, 2022


Zoezi la Uhakiki wa Wateja: Tunafanya uhakiki wa wateja wetu na kwa kuanzia tumeanza na wateja wanaohudumiwa na Ofisi ya Kanda ya Mjini Kati kwa lengo la kuboresha huduma. Tafadhali tuwapatie ushirikiano Maafisa watakaotembelea Kaya zetu. Maswali yatakayoulizwa ni kuhusiana na huduma ya majisafi na majitaka. Watakuwa na mavazi maalum na watakuwa na vitambulisho. Kwa ufafanuzi wasiliana nasi ama Ofisi ya Kata yako ama Mwenyekiti wako wa Mtaa.