News

Posted On: Mar, 25 2024

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI YARIDHISHWA NA UFANISI WA MRADI WA MAJI WA BUTIMBA

News Images

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI YARIDHISHWA NA UFANISI WA MRADI WA MAJI WA BUTIMBA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na ufanisi wa mtambo wa kuzalisha na kutibu maji wa Butimba Mkoani Mwanza na imepongeza jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kufanikisha mradi huo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Japhet Hasunga amesema hayo Machi 23, 2024 mara baada ya kutembelelea na kukagua shughuli ya uzalishaji maji inayoendelea sambamba na hatua mbalimbali za ukamilishwaji wa mradi wa maji wa Butimba.

“Kwa tulichokiona kinavutia na kinafurahisha, tumeanzia pale maji yanapochotwa ziwani hadi hatua ya mwisho ambapo majisafi na salama yanaruhusiwa kufika kwa wananchi; kwa tulichokiona kwa macho ni kitu kizuri, ni mradi mzuri,” amepongeza Mhe Hasunga.

Amebainisha lengo la ziara ya Kamati katika mradi huo ni kushuhudia uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kutazama namna ambavyo fedha ya Serikali inavyotumika katika utekelezaji wa miradi.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Mhe. Ellen Bogohe ameshukuru Kamati kutembelea mradi huo ambao amesema ni wakipekee kuwahi kujengwa Nchini.

“Tunashukuru kwa kuja kuangalia huu mradi, ni kweli mradi unavutia kama mlivyosema, changamoto zilikuwa nyingi lakini kwa umahiri wa Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa fedha nyingi ili kupunguza adha kwa wananchi, tuanaahidi kupitia mipango tunayoendelea nayo huduma itakuwa imesambaa maeneo mengi zaidi,” amefafanua Bogohe.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Ndg. Neli Msuya ameelezea hali halisi ya uzalishaji maji, mahitaji yaliyopo na mipango inayoendelea kutekelezwa na Serikali.

Amesema Mradi umekamilika kwa asilimia miamoja na uzalishaji unafanyika kulingana na usambazaji unavyokwenda na kwamba hatua zinazoendelea ni za kuboresha mifumo ya usambazaji maji ili kufikia wananchi wengi zaidi kadri ambavyo mradi ulivyotarajiwa kufika.

“Chanzo kimekamilika na kazi inayofanyika sasa ni ya kulaza mabomba ya kusambaza maji. Ipo mikakati ya kuweza kuboresha huduma za maji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu mikuu ya kusambaza maji kwa maana ya kuongeza mtandao wa bomba, kujenga matenki ya kuhifadhi maji ili maji kufikia wananchi wengi na hasa waishio milimani,” amesema.

Amesema ili kufikisha huduma ya maji kwa uwiano katika maeneo tarajiwa, mradi wa ujenzi wa matenki unakwenda kuanza hivi karibuni.

“Maeneo yantakayokuwa na matenki yatakayopokea maji haya ya Butimba ni Kisesa (lita milioni tano), Nyamazobe (lita milioni tano), Buhongwa (lita milioni 10), Fumagila ya Juu (Kishiri) (lita milioni 10) na Usagara (lita milioni moja),” amefafanua Neli.

Mbali na ujenzi wa matenki hayo, Neli amesema MWAUWASA inatarajia kukarabati na kupanua Mtambo wa Kuzalisha maji wa Capripoint