News

Posted On: Jan, 28 2025

KITENGO CHA HABARI MWAUWASA CHAZURU AUWSA

News Images

Timu ya Maofisa kutoka kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano MWAUWASA imefanya ziara ya siku mbili Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA) kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya kiutendaji.

Katika ziara hiyo Wataalamu wa Mawasiliano na Uhusiano kutoka MWAUWASA na AUWSA wamejadili na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ikiwemo mbinu za kuimarisha Mawasiliano na Uhusiano na Wadau katika sekta ya maji.

Aidha, Wataalam hao pia wamepata nafasi ya kutembelea Makundi mbalimbali ya Wateja wanaohudumiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha na kujionea ushirikishwaji wa wananchi katika huduma muhimu ya maji na usafi wa Mazingira.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano AUWSA Marry Maleko amesema ziara hizo ni muhimu kwani ni chachu ya kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Watendaji na kuboresha utendaji ili kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.