News

Posted On: Apr, 03 2024

MABORESHO YA MIUNDOMBINU YANAENDELEA

News Images

MABORESHO YA MIUNDOMBINU YANAENDELEA

Kazi ya Maboresho ya Mtandao wa bomba la kusambaza maji Bulale-Kigoto na Nyangwi inaendelea kutekelezwa na Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA).

Kazi iliyofanyika ni pamoja na uwekaji wa 'air valves' katika mfumo na kazi inayoendelea ni uchomaji wa bomba la inchi 4 kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji katika maeneo hayo.

Aidha, maboresho hayo yatasaidia kurahisisha kufikiwa na huduma ya maji kwa muda mfupi pindi huduma itakapoelekezwa katika maeneo hayo.

Maboresho haya yanafanyika kufuatia ziara ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Ndg. Neli Msuya Machi 24, 2024 alipotembelea maeneo ya Bulale na Kigoto Kata ya Buhongwa ili kukagua mwenendo wa upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo hayo.

Katika ziara hiyo, Ndg. Neli aliahidi wakazi wa maeneo hayo kuwa jitihada za kuimarisha upatikanaji wa huduma zitafanyika mapema iwezekanavyo ili kuboresha huduma kwa awamu.

Alielekeza timu ya ufundi inayosimamia usambazaji maji kuhakikisha huduma inaimarika kwa kulaza bomba kubwa zaidi la inchi 4 ili kukidhi mahitaji yanayotokana na ongezeko la wakazi na shughuli za maendeleo katika maeneo hayo.

#kaziinaendelea💦