News

Posted On: May, 04 2024

MAKABIDHIANO YA VYOO JAMHURI SHULE YA MSINGI

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) ikishirikiana na wafadhili VEI pamoja na Rotary Club imekabidhi jengo la vyoo katika Shule ya Msingi Jamuhuri iliyopo Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Vyoo hivyo vimekabidhiwa na Ndugu Linda Baas, muwakilishi wa Rotary Club Tanzania, wafadhili wa mradi huo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vyoo hivyo, Ndugu Linda Baas amesema mradi utaimarisha hali ya Usafi wa Mazingira katika shule na pia kubadilisha tabia za watoto katika kuboresha Mazingira mashuleni.

“Katika Mradi huu wa vyoo tumeweka pia Matenki ya maji, hii itasaidia upatikanaji wa maji wa uhakika kwa watumiaji wa vyoo hivyo pia kwa kunawa mikono kwa Majisafi tiririka na sabuni ili kulinda afya zao kama muongozo wa afya unavyoelekeza,” ameeleza

Baada ya kukabidhi vyoo hivyo, Mhe. Diwani Rosemary Mayunga amepongeza MWAUWASA kwa mradi ambapo amesema utakwenda kuwa msaada katika kuimarisha hali ya usafi wa Mazingira.

“Pongezi kubwa kwao MWAUWASA pamoja na wafadhili kwa mradi huu wa vyoo vya mfano pamoja na miradi mingine inayoendelea kutekelezwa katika wilaya yetu mmejenga vyoo hivi kwa ubora na tunaahidi tutavitunza ili vidumu na kuendelea kuwa msaada kwa watumiaji” amesema

Naye, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jamuhuri Ndugu Mussa Ramadhani amesema Mradi umekuwa msaada mkubwa katika shule

“Tunaahidi kutoa ushirikiano na kuwa mfano bora katika utunzaji wa vyoo katika Jiji na Tanzania nzima kwa ujumla," amesema.

Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Vivien Temu alitoa elimu kwa wanafunzi juu ya usafi wa mazingira na jinsi ya unawaji mikono pindi wanapotoka chooni kwa majisafi na sabuni.

Akielezea slogani kwa wanafuzi isemayo

“Mabadiliko lengo letu vyoo safi, furaha yetu”