News
MRADI WA QUICK WIN AWAMU YA PILI WAENDELEA KUTEKELEZWA KWA KASI

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza ( MWAUWASA) Ndugu. Neli Msuya amekagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Matokeo ya haraka ( Quick Win ) awamu ya pili ambao unaendelea kutekelezwa kata ya Buhongwa, Mkolani na Luchelele Wilayani Nyamagana.
Ndugu.Neli amefanya ziara hiyo Aprili 22, 2025 akiwa ameambatana na Timu ya wataalam kutoka MWAUWASA.
MWAUWASA inaendelea na utekelezaji wa Miradi mbalimbali kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wakazi wa maeneo yanayohudumiwa.
Mradi huu umefikia asalimia 90 na kazi iliyopo sasa ni kuongeza kina cha mitaro katika maeneo yenye miamba na ulazaji wa bomba unaendelea kwa kasi katika maeneo mbalimbali ya kata hizo na hadi sasa zoezi la ulazaji wa bomba kwa km 39.5 imekamilika.
Kukamilika kwa Mradi huo kutaimarisha upatikanaji wa huduma ya Majisafi kwa wakazi zaidi ya 48000 wa maeneo ya Buhongwa Magharibi, Miti mirefu, Buhongwa Mashariki, Shibayi, Bulale, Kigoto, Nyanembe, Nyamatala, Nyakangwe, Ng’washi, Mkolani darajani, Nyahingi, Shadi, Nyakalekwa, Nyanza na ihumilo.
Mwauwasa inaendelea kuishukuru Serikali inayoongozwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma ya Maji Mwanza.