News

Posted On: Apr, 17 2024

MWAUWASA& KASHWASA KUSHIRIKIANA NA HAMBURG WASSER

News Images

MWAUWASA& KASHWASA KUSHIRIKIANA NA HAMBURG WASSER

Katika kuhakikisha huduma ya majisafi na usafi wa Mazingira zinaendelea kuimarika Nchini, Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) na Kahama Shinyanga (KASHWASA) zimekutana na Mamlaka ya Maji ya Hamburg ya Nchini Ujerumani (Hamburg Wasser) na kujadili namna bora ya kushirikiana ili kuimarisha upatikanaji wa huduma.

Kikao hicho kimefanyika Maji House, Jijini Mwanza Aprili 13 na kushirikisha wataalam kutoka Mamlaka zote tatu ambao wamejadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano.

Miongoni mwa maeneo ya ushirikiano miongoni mwa Mamlaka hizo tatu ni pamoja na uboreshaji wa huduma ya uzalishaji maji katika vyanzo vya Butimba, Capripoint, Nyahiti, Busulwa na Ihelele kwa gharama nafuu, pia kuona namna ya kupunguza matumizi ya nishati sambamba na maboresho ya vituo vya tiba ya majitaka.

Katika kutimiza azma ya Serikali ya kumpatia mwananchi huduma bora, endelevu na yenye kutosheleza, Mamlaka za Maji zinaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wa Maendeleo kutoka Nchi mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha azma hiyo inafikiwa kikamilifu.