News

Posted On: Sep, 22 2023

​MWAUWASA KUBORESHA HUDUMA YA MAJI NYEGEZI

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imekabidhi shehena ya mabomba yenye urefu wa Km 2 kwa uongozi wa uongozi wa mtaa wa Ng'washi, Kata ya Buhongwa ikiwa ni sehemu ya jitihada za Mamlaka za kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa jiji la Mwanza,

Mabomba hayo yenye ukubwa wa inchi 3, inchi 2 na inchi 1 yamekabidhiwa kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo ya Buhongwa mashariki,Nyaluhama, Ng'washi, Nyanembe na Buhongwa magharibi.

Kazi ya ulazaji wa mabomba hayo itafanyika kwa lengo la kusogeza huduma ya maji karibu kwa wakazi wa maeneo ambao wako mbali na miundombinu ya maji pamoja na kuboresha miundombinu chakavu.