News

Posted On: Aug, 12 2025

MWAUWASA MAGU YAWAKUMBUKA WAHITAJI S/M ITUMBILI

News Images

MWAUWASA kanda ya Magu imetoa msaada wa mahitaji kwa Shule ya Msingi Itumbili iliyopo Wilayani Magu inayowahudumia watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo wenye ualbino, viziwi na changamoto nyingine za kimaumbile.

Msaada huo umetolewa kama sehemu ya mchango wa MWAUWASA kwa jamii, hasa katika kuunga mkono elimu jumuishi na kuboresha mazingira ya wanafunzi hao kujifunza kwa staha na furaha.

Wakizungumza wakati wa tukio hilo, maafisa wa MWAUWASA wamesema lengo ni kuonesha mshikamano na kuwahamasisha wadau wengine kuunga mkono juhudi za shule hiyo inayotoa elimu kwa watoto wanaohitaji uangalizi wa kipekee na wahitaji wengine katika jamii.

Uongozi wa shule umetoa shukrani kwa MWAUWASA kwa moyo huo wa kujali, na kuomba misaada kama hiyo iendelee ili kusaidia mahitaji ya kila siku ya wanafunzi.