News

Posted On: Jul, 01 2024

MWAUWASA YASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI YA MAENDELEO KATA YA NYAMHONGOLO

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA)imeshiriki kikao cha kamati ya maendeleo kata ya Nyamhongolo kilichofanyika katika ofisi za kata hizo juni 29, 2024.

Katika kikao hicho Maafisa maendeleo ya jamii wa MWAUWASA wakiambatana na wataalamu wa wengine wamewaeleza viongozi hao kuhusu hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika kata hiyo, changamoto ya wizi na upotevu wa maji, kushamiri kwa wizi wa mita za maji pamoja na taarifa ya changamoto ya uzalishaji maji katika vyanzo vya MWAUWASA inayotokana na kuyumba kwa nishati ya umeme katika mitambo ya kuzalisha na kusukuma maji kufuatia taarifa ya TANESCO iliyotolewa juni 22, 2024

Pamoja na mambo mengine wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao hicho viongozi wa kata hiyo wameipongeza MWAUWASA kwa kujenga miundombinu ya vyoo katika shule ya msingi Nyamhongolo iliyosaidia kuimarisha hali ya usafi wa mazingira shuleni hapo.