News

Posted On: May, 02 2024

MWAUWASA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEIMOSI 2024

News Images

MWAUWASA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEIMOSI 2024

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA ) wakiwa katika shamrashamra za Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Meimosi) kwa Mwaka 2024 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Katika Maadhimisho hayo Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda amewasihi Wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uadilifu huku wakiweka uzalendo mbele katika utendaji kazi wao.

Kwa mwaka huu (2024) Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Jijini Arusha huku kwa Mkoa wa Mwanza yakifanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu inasema "Nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha."