News

Posted On: Nov, 09 2023

MWAUWASA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA TEHAMA

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imeshiriki mkutano wa Saba wa wataalam wa TEHAMA Tanzania kujadili na kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kuimarisha utendaji kazi kwa kutumia teknolojia.

Mkutano huo wa siku tano umefanyika kuanzia Oktoba 16, 2023 hadi Oktoba 20, 2023 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kukutanisha wadau wa masuala ya TEHAMA kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Estonia, Marekani (USA) na Nchi za Afrika Mashariki.

Mkutano na Tume ya TEHAMA Tanzania (ICT Commission Tanzania) ulifunguliwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (Mb).

Kaulimbiu ya mkutano kwa mwaka huu ni "Kuibua teknolojia zinazoibukia katika mageuzi ya kidijitali kwa ajili ya kubuni nafasi za kazi na maendeleo ya kijamii na kiuchumi" ikilenga kuleta mageuzi ya kidijitali katika utoaji wa huduma kwa taasisi na mashirika ya Umma na binafsi ikiwemo MWAUWASA ili kwenda na kasi ya maendeleo ya teknolojia duniani.