News
NYEGEZI WAHAMASISHWA KULIPA ANKARA ZA MAJI KWA WAKATI

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza MWAUWASA wameendelea na zoezi la makusanyo kwa kufuatilia malipo ya huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika eneo linalohudumiwa na Kanda ya MWAUWASA - Nyegezi.
Operesheni hiyo imeifikia Mitaa ya Majengo, California, Team, Password, Passion, Nyabuloboya, Stendi kuu ya Nyegezi, Buguku, Buguku, Majengo Mapya, Mkolani naaeneo mengine yanayohudumiwa na Kanda hiyo.
Aidha, zoezi hilo limeongozwa na Mkurugenzi wa Fedha MWAUWASA CPA Nyanjige Ngambeki pamoja na Watumishi kutoka Ofisi kuu na Ofisi za Kanda ya Nyegezi ambapo ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa kutimiza wajibu wao wa kulipia ankara zao kwa wakati.
"Wakati Serikali ikiendelea kujitahidi kuimarisha na kuboresha huduma hii muhimu ya maji, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuunga mkono jitihada hizi kwa kulipia matumizi ya huduma kwa wakati ili kuwezesha Mamlaka kujiendesha na kuendelea kuboresha huduma zaidi'. Amesisitiza.