News

Posted On: Apr, 03 2024

​​WANANCHI WASHIRIKI MABORESHO YA HUDUMA YA MAJI BUGOGWA

News Images

WANANCHI WASHIRIKI MABORESHO YA HUDUMA YA MAJI BUGOGWA

Wananchi wa Mtaa wa Lugezini katika Kata ya Bugogwa wakishiriki katika zoezi la ulazaji bomba kwa ajili ya kuboresha huduma ya usambazaji maji katika mtaa huo.

MWAUWASA inaendelea na zoezi la uboreshaji wa mifumo ya usambazaji maji kwa maeneo yaliyokuwa hayajafikiwa kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuongezwa kwa mtandao wa bomba pamoja na ujenzi wa vituo vya kuchotea maji (Gati/DP) kwa baadhi ya maeneo ya pembezoni yenye upungufu wa huduma.

Kwa mtaa wa Lugezini hadi sasa jumla ya Gati 04 zimejengwa kwaajili ya kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi wa maeneo hayo ambapo zaidi ya Wananchi 3,883 watanufaika na mradi.