News

Posted On: Apr, 19 2024

​Watumishi wa Sekta ya Maji watakiwa kutumia TEHAMA kuboresha kazi

News Images

Watumishi wa Sekta ya Maji watakiwa kutumia TEHAMA kuboresha kazi

Watumishi wa Sekta ya Maji kote nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia ipasavyo TEHAMA ili kuboresha utendaji kazi, hivyo kuimarisha huduma kwa wananchi wanaowahudumia.

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Wizara ya Maji Bi. Wanyenda Kutta amesema hayo katika kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA)

"Serikali imeturahishia utendaji kazi wetu kwa kutuletea mifumo mizuri ya TEHAMA; tuhakikishe tunaitumia ipasavyo kwa lengo la kuimarisha utendaji wetu kwa manufaa ya wananchi tunaowahudumia, twende na wakati, tusirudi nyuma," Bi. Kutta amesema

Akitolea mfano mfumo wa MAJIS, amesema umebuniwa kurahisisha uendeshaji, usimamizi na udhitibi wa mapato ya Mamlaka na Bodi za Maji za Mabonde na kusisitiza kuwa unapaswa utumike kikamilifu ili kuleta tija iliyokusudiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Bi. Neli Msuya amepongeza utaratibu huo wa Wizara kwa Wakurugenzi wake kutembelea taasisi zake na kutoa elimu na maelekezo ya namna bora ya uendeshaji wa taasisi ili kuimarisha huduma kwa wananchi.

"Ni utaratibu mpya wa Wizara kwa Wakurugenzi wake kututembelea, tumepokea maelekezo na tunaahidi kuyatekeleza bila kuchelewa na pia tunashukuru kwa elimu mliyotupatia imetuhamasisha kuongeza jitihada katika utendaji wetu kwa manufaa ya Taifa letu," Bi. Neli amesema.

Mkurugenzi Bi. Kutta akiwa Mkoani Mwanza, alipata fursa ya kuzungumza na watumishi wa RUWASA, Ofisi ya Bonde la Ziwa Victoria na Maabara ambapo amesisitiza umuhimu wa taasisi zilizochini ya Wizara ya Maji kufanya kazi kwa kushirikiana.