News
WAZIRI AWESO AIPONGEZA MWAUWASA, ATOA MAAGIZO MATATU KWA MENEJIMENTI MPYA
WAZIRI AWESO AIPONGEZA MWAUWASA, ATOA MAAGIZO MATATU KWA MENEJIMENTI MPYA
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, amewapongeza watumishi wa MWAUWASA kwa kuendana na mabadiliko ya kiutendaji, hatua ambayo amesema imeanza kuleta matokeo chanya katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza jana katika kikao cha kiutendaji na watumishi wa MWAUWASA, Mhe. Aweso ameipongeza timu maalum ya Wizara ya Maji iliyosimamia kipindi cha mpito ikiongozwa na Mhandisi Mashaka Sitta, huku akimtambulisha rasmi Mhandisi Leonard Msenyele kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa MWAUWASA.
Waziri Aweso pia ametoa maagizo matatu kwa menejimenti mpya: kuharakisha ukamilishaji wa miradi inayoendelea kutekelezwa, kupunguza upotevu mkubwa wa maji na kusimamia uwajibikaji wa watumishi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, amesisitiza maadili, nidhamu na uwajibikaji, huku Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Amiri Mkalipa aliye muwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiahidi ushirikiano wa Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya maji na akigusia kuhusu mpango wa kuanzisha kampeni maalum chini ya ofisi ya mkuu wa mkoa kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaojihusisha na wizi wa maji .