News

Posted On: Nov, 10 2022

ZIARA YA MKUU WA MKOA BUTIMBA

News Images

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa Dakio jipya la Maji katika chanzo kipya cha Maji cha Butimba ili kujionea hali halisi ya ujenzi wake.

Ziara hiyo ya Novemba 8, 2022, ililenga kukagua na kujionea hali halisi ya utekelezaji wa mradi sambamba na kuzungumza na Mkandarasi Kampuni ya SOGEA SATOM kutoka Ufaransa.

Katika ziara hiyo, Mhe. Malima ameielekeza MWAUWASA kufanya tathmini makini kuhusiana na idadi halisi ya wakazi wa Jiji la Mwanza ili miradi yake ya maji iwanufaishe wananchi wote.

Ameielekeza MWAUWASA kuongeza jitihada za kuzuia upotevu wa maji na kuboresha mfumo wa usambazaji maji ili kuwaondolea adha wananchi hasa ilizingatiwa kuwa maji mengi yanayozalishwa yanapotea kabla hayajamfikia mwananchi.

Katika ziara hiyo, Mhe. Malima aliambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza.