CHANGAMKIA OFA YA SIKUKUU KUTOKA MWAUWASA
Posted On: Dec 24, 2025
Msimu huu wa sikukuu za Christmass na mwaka mpya, MWAUWASA imetoa offa kwa wateja wake waliositishiwa huduma ya maji kwa sababu ya madeni ya bili. Lipia kiasi cha deni bila ada ya marejesho (TZS 15,000/=) kisha urejeshewe huduma kwa makubaliano maalum ya kulipa kidogokidogo kumalizia deni huku huduma ikiwa imesharejeshwa.
Ofa imeanza tarehe 1 hadi 31 Desemba 2025.
Tembelea ofisi za kanda zilizo karibu nawe ama tupigie simu namba 0800110023 bila malipo