MATENGENEZO YA KONA YA BWIRU YAKAMILIKA, HUDUMA YAANZA KUREJEA

Posted On: Aug 29, 2023


MATENGENEZO YA KONA YA BWIRU YAKAMILIKA, HUDUMA YAANZA KUREJEA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) inawataarifu wateja wa maeneo ya Kilimahewa, Selemani Nasorr, Nyamanoro, Pasiansi, Iloganzara, Ilemela, Lumala, Kiseke yote, Mondo, Bwiru, Kitangili, baadhi ya maeneo ya Buswelu na baadhi ya maeneo ya Kirumba kuwa matengenezo yaliyokuwa yanafanyika katika bomba la inchi 20 katika eneo la Kona ya Bwiru yamekamilika saa 3:30 usiku na huduma ya maji imeanza kurejea kwenye maeneo mbalimbali. Huduma itaendelea kuimarika kwenye maeneo mengine kadiri maji yanavyosafiri.

Mamlaka inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kupitia 0800110023 bure