News

Posted On: Mar, 08 2024

HUDUMA IMEIMARIKA IGOMBE

News Images

Wakazi wa Igombe Kata ya Bugogwa wamefurahishwa na huduma ya majisafi na salama itolewayo na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA).

Wamebainisha hayo Machi 1, 2024 Mtaa wa Igombe A kwa nyakati tofauti kufuatia maboresho yanayofanywa na MWAUWASA ya kuhakikisha wanapata huduma endelevu katika maeneo yao.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Balozi wa Mtaa Mzee Patrice Dede ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufikishiwa huduma ya maji na MWAUWASA.

"Namshukuru sana Rais kwa kutujali sisi watu wa Kata ya Bugogwa hususan Mtaa wetu wa Igombe A, MWAUWASA imetufikia," amesema Mzee Dede.

Kwa upande wake Bibi Shundu amebainisha kuwa kusogezwa kwa huduma ya maji katika eneo lake kutampunguzia adha ya kufuata maji ziwani ambayo amesema hayakuwa safi wala salama hasa ikizingatiwa kuwa shughuli nyingi za kibinaadamu zinafanyika maeneo ya kando ya ziwa walipokuwa wakichota maji.

"Kusogezwa huduma ya maji katika eneo hili ni msaada mkubwa kwetu; tuliteseka kwa muda mrefu," amesema.

MWAUWASA inahudumia Kata ya Bugogwa na Kayenze zilizoko pembezoni mwa Wilaya ya Ilemela ambapo hatua mbalimbali za maboresho zinaendea.

#kaziiendelee🔥🔥🇹🇿🇹🇿🇹🇿💪🏿💪🏿💪🏿💪🏿