News

Posted On: Sep, 22 2023

KAYA 1100 KUNUFAIKA NA MTAMBO WA IHILA B

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imefanya majaribio katika mtambo wa kusukuma maji Ihila kwa lengo la kupima ufanisi wake.

Mtambo wa Ihila umejengwa kwa fedha za miradi ya Uviko 19 ukilenga kuhudumia kaya 1100 kutoka maeneo ya Ihila B Mlimani, Ihila B chini, Nyakagwe, Ng'washi, Ihila A, Gwajima na Agape. Mtambo wa Ihila una uwezo wa kusukuma lita 1,500,000 kwa masaa 20 na kupeleka maji kwenye matenki ya lita 50,000 ili kusaidia kufikisha huduma ya maji kwa maeneo husika.

Tayari majaribio ya kuwasha pampu ili kuona msukumo wa maji yamefanyika leo tarehe 21 na maboresho mbalimbali yanaendelea.