News
MAFUNZO YA MIFUMO YA UKUSANYAJI DATA ZA WATEJA WA MWAUWASA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza MWAUWASA inaendelea na zoezi la uboreshaji wa taarifa za Kijiographia za miundombinu kupitia Mfumo wa GIS (Geographic Information System) kwa lengo kuongeza ufanisi na kuendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Katika hatua hiyo, Wataalam wa Mfumo huo wa GIS MWAUWASA wameendesha mafunzo kwa Wataalam wa Kada ya Ufundi kanda ya Nyegezi ili kuwajengea uwezo wa kutumia mifumo ikiwa ni hatua ya awali katika zoezi la kuhakikisha miundombinu yote ya Wateja wapya inaingizwa katika ramani kuu ya maungamisho mapya ya huduma (New connection Map).
"Zoezi hili litasaidia kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kurahisisha kazi za kiufundi ikiwemo maboresho ya miundombinu kama ubadilishaji wa mabomba na kuwa na taarifa sahihi za miundombinu". Ameeleza Clifford Majinji Mtaalam wa Mfumo wa taarifa za Kijiografia (GIS) MWAUWASA
"Baada ya kukamilisha zoezi hili hapa katika Kanda ya Nyegezi, tunatarajia kuendesha mafunzo haya katika maeneo yote ya Kanda za kihuduma za MWAUWASA kwa Wataalam wenzetu wa kada ya ufundi ili tuendelee kutekeleza majukumu yetu ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi" amesema Denis Mauya Mtaalam wa (GIS) MWAUWASA.