News

Posted On: Oct, 01 2024

​MBUNGE WA NYAMAGANA ASHIRIKI KAMPENI YA MWAUWASA MTAA KWA MTAA - " SEMA USIKIKE"

News Images

MBUNGE WA NYAMAGANA ASHIRIKI KAMPENI YA MWAUWASA MTAA KWA MTAA - " SEMA USIKIKE"

Mbunge wa jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ameshiriki katika kampeni ya MWAUWASA mtaa kwa mtaa inayolenga kufuatilia upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Katika ziara iliyofanyika katika kata za Buhongwa na Lwanima Mh Mabula akiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA Neli Msuya na Watalamu kutoka MWAUWASA wametembelea mitaa ya Sahwa ya chini, Sahwa ya Juu, Semba pamoja na Kagera.

"Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt Samia kwa kuwezesha mradi wa dharura, lakini pia kwa kutupa msimamizi wa Wizara hii Mhe. Jumaa Aweso mchapakazi na anayewapenda watu, Mara ya mwisho tulikua naye hapa na tukakesha

hadi mitambo ya mradi huu ikawashwa kuanza majaribio, leo hii tunashuhudia maji yamefika kwa Wananchi" ameeleza Mhe. Mabula.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA ametoa shukrani kwa wananchi na viongozi kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Mtaa kwa ushirikiano wanaotoa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali, na kueleza kuwa, MWAUWASA inaendelea na miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 10 ya kuboresha huduma wakati mradi mkubwa wa ujenzi wa matenki makubwa ukiendelea. Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Usambaji maji na Usafi wa Mazingira Mhandisi Robert Lupoja aliongeza kuwa mbali na mradi wa dharura wa Sahwa-Buhongwa Mamlaka imejipanga kutekeleza miradi ya mpango wa muda mrefu na wa kudumu ili kuhakikisha huduma ya maji inaimarika zaidi.

Wakizungumza kwa Nyakati tofauti Wananchi na viongozi wa maeneo hayo wameishukuru Serikali kwa mradi huo na kuongeza kuwa wanayo imani kubwa ya huduma kuwa bora zaidi kutokana na jitihada zianzoendelea.

" Tulikua na changamoto kubwa eneo hili, na mwanzo tulijua ni hadithi tu lakini sasa tunajionea maji yamefika, Pongezi nyingi kwa Mhe. Rais kwa kumtua mama ndoo ya maji kichwani" ameeleza Abdallah Majaliwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kagera.