News

Posted On: Jan, 17 2024

MKUTANO WA WADAU WA MRADI WA VYOO MASHULENI MKOANI MWANZA

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kwa kushirikiana na Shirika la Maji la Uholanzi maarufu kama Vitens Evides International (VEI) na Shirika la Kutoa Huduma Duniani (ROTARY) wamefanya mkutano wa ushirikishwaji wa Wadau katika ujenzi wa Mradi wa vyoo katika shule za Msingi Wilaya ya Ilemela na Nyamagana.

Mradi umelenga kujenga vyoo kumi (10) katika shule za msingi wilaya ya Nyamagana na Ilemela chini ya ufadhili wa VEI na ROTARY.

Katika mkutano huo, Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Bw. Balandya Elikana amewashukuru wafadhili VEI na ROTARY kwa ufadhili huo wa kujenga vyoo katika shule za msingi na pia amewapongeza wote waliofanikisha uwepo wa mradi.

Amesisitiza kuanza kwa utekelezwaji wake mapema iwezekanavyo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali za kuimarisha afya ya wananchi wake

Akizungumza wakati wa mkutano huo Ndg. Linda Baas ambaye ni mwakilishi wa wafadhili wa mradi (VEI na ROTARY) amesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika miradi ya kijamii

“Katika mradi huu wa vyoo tumelenga kujenga vyoo 10 katika wilaya zote mbili, Nyamagana shule 5 na ilemela shule 5,” amefafanua Linda

Shule ambazo zitanufaika na mradi huu ni pamoja na Shule ya msingi Jamhuri, Nyafla, Nyamanoro, Isenga na shule ya msingi Buzuruga C na D kwa upande wa Ilemela na kwa upande wa Nyamagana ni Shule ya Msingi Nyanza, Kanindo, Mandela, Sahwa na Shule ya Msingi Bujingwa.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Ndg. Neli Msuya alishukuru wadau na washirika wa maendeleo kwa kufanikisha zoezi hilo.

Ndg. Neli ameahidi kutoa ushirikiano kwa kila hatua ya utekelezaji wa mradi