News

Posted On: Sep, 22 2023

MWAUWASA KAZINI UBORESHAJI MIUNDOMBINU

News Images

Watumishi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) wakifanya tathmini (survey) eneo la Kishiri ikiwa ni hatua ya maandalizi kabla ya kuanza kwa zoezi la kupanua na kuboresha mtandao wa huduma ya maji.

Kazi ya upanuzi wa mtandao wa maji eneo la Kishiri inalenga kuboresha miundombinu ili kuendana na ongezeko la maji yatakayozalishwa baada ya kukamilika kwa mradi mpya wa maji Butimba.

Kazi ya tathmini (survey) hufanyika kama hatua ya awali kabla ya shughuli za uchimbaji na ulazaji kuanza kutekelezwa ili kupata taarifa sahihi ya mahitaji yanayohitajika kwa ajili ya kazi hizo.