News

Posted On: Nov, 27 2023

MWAUWASA KUBADILISHANA UZOEFU NA MAMLAKA YA MAJI YA HAMBURG - UJERUMANI

News Images

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) wametembelea Mamlaka ya Maji ya Hamburg- Ujerumani kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika uzalishaji na usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira.

Ziara ya watumishi hao ilianza rasmi Novemba 20 na kuhitimishwa Novemba 24, 2023 ambapo walipata fursa ya kutembelea katika Maabara ya maji, eneo la tiba ya majitaka, mtambo wa kuzalisha maji na kuyatibu pamoja na karakana ya mita za maji.

MWAUWASA inaendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha huduma ya maji inaendelea kuimarika.

#Kaziinaendelea 💦