News
Posted On:
Dec, 12 2024
OPERESHENI DHIBITI MIVUJO YA MAJI
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) wameendesha zoezi la kuzungukia maeneo mbalimbali Jijini Mwanza kwa lengo la kubaini na kudhibiti mivujo ya maji katika miundombinu ya maji ya Mamlaka.
Zoezi hilo ni mwendelezo wa Kampeni maalum ya kukagua miundombinu ya maji na kudhibiti mivujo ili kuepusha uvujaji maji na kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
MWAUWASA inawaomba wananchi kuunga mkono juhudi hizo kwa kutoa taarifa za mivujo ya maji waonapo hitilafu katika Miundombinu ya maji ya MWAUWASA.