News

Posted On: Sep, 17 2025

REGIDESO - BURUNDI YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO MWAUWASA

News Images

Wataalamu kutoka *Mamlaka ya Maji na Umeme ya REGIDESO* nchini Burundi, wamefanya ziara ya kikazi katika *Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA)* kuanzia *tarehe 01 hadi 04 Septemba 2025*, kwa lengo la *kubadilishana uzoefu na kujifunza namna ya utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa maji* katika Jiji la Mwanza.

Katika ziara hiyo, wataalamu hao walipata fursa ya kutembelea *kurugenzi na vitengo mbalimbali vya MWAUWASA*, vikiwemo *Huduma kwa Wateja, Usambazaji Maji, Raslimali Watu* pamoja na *maeneo ya kutibu maji na matanki ya kuhifadhia maji*.

Aidha, walitembelea *mradi mkubwa wa ujenzi wa matenki matano*, unaohusisha tenki la *Buhongwa, Usagara* na *Kisesa*, yatakayopokea maji kutoka *Mradi wa Butimba*.

Akizungumza mmoja wa Wataalam hao *Ndugu Noel Nahimana*, Mratibu wa Mradi kutoka REGIDESO, aliishukuru MWAUWASA kwa mapokezi na ushirikiano mzuri walioupata wakati wa ziara yao.

“Kiukweli tumejifunza
mambo mengi sana, hususani upande wa usambazaji wa maji. Ujuzi tulioupata tunaenda kuuendeleza kwa vitendo kwetu Burundi,” alisema Noel.

Wataalamu hao pia wameipongeza *Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watumishi wa MWAUWASA* kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuboresha miundombinu ya maji katika Jiji la Mwanza, hali inayosaidia kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.