News
TAASISI YA MTETEZI WA MAMA MKOA WA MWANZA YAUNGA MKONO UTUNZAJI WA VYAZO VYA MAJI

Taasisi ya Mtetezi wa Mama Mkoa wa Mwanza imefurahishwa na uendeshaji wa Mradi wa Maji Butimba na kuipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa uwekezaji mkubwa uliyofanyika.
Haya yamesemwa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bi. Minael Mndeme walipotembelea Mradi huo kwa lengo la kujionea utendaji kazi wake na uungaji mkono juhudi za utunzaji wa vyanzo vya maji kwa kupanda miti katika chanzo hicho.
“Kwa kweli tumefurahishwa sana na Mradi huu kwani tumeona mengi ya kujifunza kupitia Mradi huu unaofanya kazi kwa teknolojia ya kisasa kabisa, kuanzia Maji yanavyozalishwa na yanavyotibiwa.
“Tuipongeze Serikali inayoongozwa na Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji huu mkubwa, kwa kweli mama anastahili mitano tena”, ameeleza Bi. Minael
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano MWAUWASA Vivien Temu amesema Mradi huo kwa sasa umetekelezwa kwa awamu ya kwanza na unauwezo wa kuzalisha lita za Maji Milioni 48 kwa siku na unahudumia maeneo mbalimbali ikiwemo Maeneo ya Butimba, Nyegezi, Buhongwa, Igoma, Kisesa, Kishiri, Mkolani, Luchelel, Sahwa na maeneo mengine.