News

Posted On: Sep, 25 2023

TUNAZINGATIA UBORA WA MAJI

News Images

Wataalam kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) wakifanya majaribio mbalimbali kwa ajili ya kuzingatia ubora wa maji yanayofika kwa wateja.

Sehemu ya majaribio hayo yanahusisha kubaini kiasi cha dawa kinachohitajika kutumika wakati wa kutibu maji (Jar Test experiment), kupima ubora na usafi wa maji (Turbidity) katika tenki kabla ya kwenda kwa watumiaji.

MWAUWASA inahakikisha kuwa maji yanayofika kwa wateja yanakidhi viwango vya ubora vinavyotakiwa kwa ajili ya matumizi ya mwanadamu.