News
WANANCHI WA IGOMBE WAMSHUKURU MHE. RAIS
Utekelezaji wa *Mradi wa Uboreshaji wa Chanzo cha Maji Igombe* umeendelea kupiga hatua ambapo sasa umefikia *asilimia 87* ya utekelezaji, Mradi huu ni miongoni mwa jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Maji katika kuhakikisha wananchi walioko pembezoni wanapata huduma bora ya majisafi na salama.
Kazi zilizofanyika hadi sasa ni:
- *Ujenzi wa jengo la chujio* (filtration unit).
- *Ununuzi wa pampu mbili* za kusukuma maji kwenye sump (chujio)
- *Ununuzi wa tanki la maji aina ya GRP* lenye ujazo wa lita 100,000.
Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi *Oktoba 2025* na utakuwa mkombozi kwa wakazi wa maeneo ya Igombe na vijiji vya jirani.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza *(MWAUWASA)* inatoa *shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania* inayoongozwa na *Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan*, kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya maji na jitihada zake za dhati za *kumtua mama ndoo kichwani*.