News

Posted On: Nov, 27 2023

​WATUMISHI MWAUWASA - NYEGEZI WAZURU MORUWASA

News Images

Watumishi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Kanda ya Nyegezi wametembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro Mjini (MORUWASA) kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika kazi.

Katika Ziara hiyo iliyofanyika tarehe 06.11.2023 watumishi wa MWAUWASA wamebadilishana uzoefu katika idara na vitengo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi katika majukumu yao ya kila siku.

Vilevile, Watumishi hao walipata nafasi ya kutembelea chanzo cha Maji Mambogo na mtambo wa kutibu maji Mafiga uliopo eneo la Mindu na kujionea utendaji kazi wake.

Baada ya ziara hiyo watumishi hao wataendelea na ziara yao katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi wao.

#Kaziinaendelea 🇹🇿💦