News

Posted On: Dec, 12 2024

ZAIDI YA WAKAZI 65 NANSIO KUANZA KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJISAFI

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Kanda ya Nansio inaendelea na zoezi la ugawaji vifaa vya maungamisho ya huduma ya Majisafi kwa wakazi wa maeneo mbalimbali katika Mji wa Nansio Wilayani Ukerewe.

Zoezi hilo ni endelevu na katika awamu hii Jumla ya wakazi 65 wa Mji huo wataunganishiwa huduma na kuanza kunufaika na huduma ya Majisafi.

Sambamba na utoaji wa vifaa hivyo, Wananchi hao wanapatiwa elimu kuhusu Matumizi sahihi ya maji, njia za kuwasiliana na MWAUWASA pamoja na utunzaji wa miundombinu ya maji.