News
ZIARA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA VYOO S/M NYAMANORO

Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Neli Msuya, amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa vyoo katika Shule ya Msingi Nyamanoro, mradi unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya MWAUWASA na Shirika la Maji la Uholanzi (VEI).
Ziara hiyo imelenga kujionea hatua za ujenzi, kuhakikisha ubora wa miundombinu, pamoja na kuzungumza na wahusika wa utekelezaji wa mradi huo. Bi. Neli ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya kazi.
Mradi huo ni sehemu ya juhudi za MWAUWASA na VEI katika kuimarisha huduma za usafi wa mazingira kwenye taasisi za elimu na maeneo mengine.
Ujenzi wa vyoo hivyo vinavyojengwa katika shule 10 Wilaya za Ilemela na Nyamagana umezingatia mahitaji maalum ya watoto wa jinsia zote, ikiwa ni pamoja na maboresho ya miundombinu kwa wanafunzi wenye ulemavu na walimu.